• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Saudi Arabia yakanusha kufanya mawasiliano ya kidiplomasia na Iran

    (GMT+08:00) 2017-09-06 18:59:24

    Waziri wa mambo ya nje wa Saudi Arabia Bw. Adel al-Jubeir ambaye yuko ziarani nchini Uingereza amekanusha uwezekano wa kufanya mawasiliano ya kidiplomasia na Iran.

    Bw. al-Jubeir amesema, ili kuandaa hijja kwenye mji mtakatifu wa Mecca, Saudi Arabia imefanya mawasiliano na mkutano na Iran kwa lengo la kidini, ambao hauna uhusiano na siasa na haumaanishi kurejea kwa uhusiano wa kawaida kati ya nchi hizo mbili. Pia amesema, kama Iran ikitaka kuboresha uhusiano na Saudi Arabia, itatakiwa kubadili sera zake za kidiplomasia, kuacha kuunga mkono ugaidi na kuingilia mambo ya ndani ya nchi nyingine na kuheshimu sheria za kimataifa.

    Mwezi uliopita, Waziri wa mambo ya nje wa Iran Bw. Mohammad Javad Zarif alisema kuwa, baada ya kumalizika kwa hijja kwenye mji mtakatifu wa Mecca, Iran na Saudi Arabia zitafanya mawasiliano ya kidiplomasia ili kuboresha uhusiano wa pande mbili.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako