Kiongozi wa Tume ya kusimamia uchaguzi ya Umoja wa Ulaya nchini Kenya Marietje Schaake amesema kuwa kazi yao ilikabiliwa na changamoto kutokana na teknolojia iliyotumiwa na tume ya uchaguzi. Amesema uchaguzi wa Kenya ulitegemea kwa kiasi kikubwa kampuni binafsi na mifumo yao, hivyo haikuwa rahisi kwao kuelewa jinsi mifumo hiyo inavyofanya kazi.
Schaake amesema hayo baada ya Wakenya kuikosoa tume hiyo ya kimataifa kwa kuthibitisha kuwa mchakato wa uchaguzi ulikuwa huru, haki na wa wazi, licha ya makosa yaliyoonekana kwenye mchakato huo.
© China Radio International.CRI. All Rights Reserved. 16A Shijingshan Road, Beijing, China. 100040 |