• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Rais wa Zambia kudumisha amri ya kukabidhi madaraka ya ziada kwa polisi

    (GMT+08:00) 2017-09-06 19:35:08

    Rais Edgar Lungu wa Zambia amesema, hatashindwa na shinikizo kutoka mashirika ya kijamii linalomtaka kuondoa amri inayowapa polisi nguvu zaidi ya kukabiliana na ukosefu wa sheria nchini humo.

    Julai 5, Rais Lungu alitangaza hali ya dharura ya taifa ambayo iliipa polisi nguvu ya ziada kudhibiti mvutano uliotokea nchini humo kufuatia kukamatwa kwa kiongozi wa upinzani Hakainde Hichilema aliyeshtakiwa kwa uhaini.

    Amri hiyo ilipitishwa na bunge na kutekelezwa kwa miezi mitatu.

    Rais Lungu pia amesema, serikali yake inafanya juhudi kutoa silaha na vifaa vya kisasa kwa vikosi vya nchi hiyo ili kuviwezesha kutatua changamoto mpya za usalama.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako