• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Waziri mkuu wa China kufanya mazungumzo ya pili na wakuu wa mashirika makuu ya kiuchumi ya kimataifa

    (GMT+08:00) 2017-09-06 19:35:31

    Msemaji wa wizara ya mambo ya nje ya China Bw. Geng Shuang amesema, waziri mkuu wa China Bw. Li Keqiang jumanne ijayo hapa Beijing atafanya mazungumzo ya pili ya duara na wakuu wa mashirika ya fedha ya kimataifa.

    Miongoni mwa wakuu watakaohudhuria mazungumzo hayo ni pamoja na mkuu wa Benki ya Dunia Kim Yong, mkurugenzi mkuu wa Shirika la Fedha la Kimataifa Bibi Christine Lagard, mkurugenzi mkuu wa Shirika la Biashara la Kimataifa Bw. Roberto Azevedo, na mkurugenzi mkuu wa Shirika la Wafanyakazi la Kimataifa Bw. Guy Ryder.

    Viongozi hao wanatarajiwa kujadili ajenda mbalimbali ikiwemo ongezeko la uchumi, mageuzi ya mitindo, maendeleo endelevu, uwekezaji wa kibiashara, utulivu wa kifedha, ubunifu na kujiajiri na nafasi za ajira.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako