• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Mamlaka ya ushuru Uganda URA yaanza kuuza kwa mnada bidhaa za Nakumatt

    (GMT+08:00) 2017-09-06 20:25:27

    Mamlaka ya ushuru Uganda imeanza kuuza kwa mnada bidhaa za Nakumatt kama njia mojawapo ya kuokoa mamilioni ya fedha inayodai kampuni hiyo ya maduka makubwa ya rejareja.

    Mamlaka ya ushuru Uganda URA jumanne ilianza mnada wa umma kwa kuuza bidhaa zinazoharibika zinazomilikiwa na Nakumatt.

    Mauzo katika matawi mawili ya Nakumatt ya Bugolobi na Kamwokya jijini Kampla yalianza licha ya mamlaka ya ushuru ya Uganda kusema ipo kwenye majadiliano na Nakumatt kuhusu ulipaji wa deni la Sh7.3 million ($71,000.

    URA mwezi uliopita ilichukua rasmi usimamizi wa shughuli za Nakumatt nchini Uganda na kujipatia kipaumbele katika mapato yote,wakati wadeni wengine jijini Kampala na Kenya wakiwa mbioni kufukuzia malipo yao kutoka kwa Nakumatt.

    Hatua hii ilipelekea URA kuchukua matawi matatu ya Nakumatt pamoja na bohari ambalo pia ni makao makuu ya Nakumatt.

    Nakumatt inakabiliwa na matatizo makubwa ya fedha nchini Kenya na Uganda huku wadeni kadhaa wakijitokeza kudai takriban Sh130 milioni tangu mwezi Machi.

    URA jumanne ilisema itatangaza baadae siku itakayouza kwa mnada bidhaa zisizoharibika za nakumatt.URA inatarajiwa kumalizia na mnada katika tawi la Oasis ambalo pia liko jijini Kampala.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako