• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Wakulima Ruvuma waiomba serikali kuongeza tani za kununua mahindi yao

    (GMT+08:00) 2017-09-06 20:26:25

    Wakulima wilayani Songea mkoani Ruvuma wameiomba serikali kuongeza kiwango cha mahindi kutoka tani 6000 ambazo mkoa wa Ruvuma umepangiwa kununua pamoja na kuruhusu uuzaji wa mahindi nje ya nchi baada ya kuwa na ongezeko kubwa la mahindi huku serikali ikiwa imezuia kuuza mahindi nje ya nchi.

    Zao la mahindi ni zao la biashara na chakula kwa mkoa wa Ruvuma ambapo mwaka jana mkoa huo ulipangiwa kununua tani 20,000 hivyo wakulima wameiomba serikali kuongeza tani za kununua mahindi yao.

    Mkuu wa mkoa wa Ruvuma Dkt Binilith Mahenge akiwa katika ziara ya kutembelea vituo vya ununuzi wa mahindi amewaambia wakulima kuwa Hifadhi ya Taifa ya Chakula,NFRA,hawanunui mahindi kibiashara bali kwa utoshelevu wa chakula cha nchi.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako