• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • TFF ya Tanzania yaanzisha ligi ndogo ya wanawake

  (GMT+08:00) 2017-09-07 08:26:05

  Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania 'TFF', limeagiza Makatibu wa vyama vya Mikoa kutuma haraka majina ya timu bingwa wa mikoa wa soka ya wanawake kwa msimu wa 2016/17. Viongozi wa mikoa wamekumbushwa kutuma timu ili kufanya maandilizi ya haraka ya ili kufanyika kwa ligi ndogo itakayofanyika Septemba 22 hadi 29, mwaka huu.

  Ligi Hiyo ndogo inachezwa kutafuta timu mbili zitakazopanda daraja kucheza Ligi Kuu ya soka ya wanawake msimu wa 2017/2018.

  Huu ni msimu wa pili wa ligi ya wanawake kwani msimu uliopita, timu shiriki zilikuwa 12 na Mlandizi Queens ya Pwani iliibuka bingwa wa kwanza katika historia ya soka nchini.

  Mara baada ya kumalizika kwa Ligi Ndogo, TFF itaanza taratibu za kupanga kuanza kwa Ligi Kuu. Ligi Ndogo haitahusisha timu ambazo zimecheza Ligi Kuu msimu wa 2016/17.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako