• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Venus Williams afika hatua ya nusu fainali ya michuano ya wazi ya Marekani

  (GMT+08:00) 2017-09-07 08:26:48

  Mcheza tenis raia wa Marekani, Venus Williams amefanikiwa kutinga hatua ya nusu fainali ya michuano ya wazi ya Marekani (US Open) baada ya kumshinda mpinzani wake Petra Kvitov. Venus Williams ambaye ni dada wa mchezaji tenisi Serena Williams amefanikiwa kutinga hatua hiyo kwa ushindi wa jumla ya seti 6-3 3-6 7-6 (7-2) usiku wa kuamkia jana Jumatano.

  Hii ni mara ya 23 kwa Williams mwenye umri wa miaka 37 kutinga nusu fainali ya michuano mikubwa ya Grand Slam. Wiiliam anatarajia kucheza na mwanadada, Sloane Stephens katika mchezo ujao. Venus Williams anashika nafasi ya tisa katika viwango vya ubora wa mchezo huo ulimwenguni huku akifanikiwa kunyakua taji hilo la US Open kwa mara ya mwisho mwaka 2009.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako