• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Uchunguzi wa Umoja wa Mataifa waiwajibisha serikali ya Syria kwa shambulizi la kikemikali

    (GMT+08:00) 2017-09-07 08:58:55

    Wachunguzi wa makosa ya vita wa Umoja wa Mataifa wameviwajibisha vikosi vya serikali ya Syria kwa kufanya shambulizi la kikemikali lililosababisha vifo vya watu 83, theluthi wakiwa ni watoto, kwenye eneo la Khan Sheikhun mwezi Aprili. Wachunguzi hao wamesema kuwa wamepata ushahidi imara unaoweza kuthibitisha kuwa vikosi vya serikali ya Syria vilifanya shambulizi hilo lililotumia gesi ya sarin. Awali, serikali ya Syria ilikataa kuhusika na shambulizi hilo na kudai kwamba haimiliki silaha za kemikali baada ya kusaini makubaliano ya kuondoa silaha hizo mwaka 2013.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako