• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Jumuiya ya kimataifa yalaani juhudi za kuanzisha nchi mpya huko Somalia

    (GMT+08:00) 2017-09-07 09:25:28

    Jumuiya ya kimataifa imeeleza wasiwasi kutokana na ripoti za kuanzisha nchi mpya kusini mwa Somalia.

    Wawakilishi wa Umoja wa Mataifa, Umoja wa Afrika, Umoja wa Ulaya, Shirika la Maendeleo la kiserikali la nchi za Afrika Mashariki IGAD, na Marekani wamesema wanafuatilia kwa karibu maendeleo katika mkoa wa utawala maalum wa HirShabelle, kutokana na taarifa iliyotolewa na Bunge la mkoa huo kuwa limemwondoa madarakani rais wa mkoa huo Ali Abdullahi Osoble Agosti 14.

    Wawakilishi hao wamezitaka pande husika kuendelea na juhudi za kusuluhisha suala hilo muhimu kwa njia za kikatiba na kisheria, na kujizuia kufanya vitendo vyovyote vinavyoweza kuvuruga mchakato wa kujenga taifa.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako