• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Umoja wa Afrika kuunda timu itakayosimamia kuondoka kwa vikosi vyake nchini Somalia

    (GMT+08:00) 2017-09-07 09:26:10

    Umoja wa Afrika umeunda timu ya wataalam zikiwemo nchi zinazotoa askari ili kuandaa njia za kuwaondoa askari wake nchini Somalia ifikapo Mei mwaka ujao.

    Kamati ya Uratibu wa Operesheni za Kijeshi ya Kikosi cha Kulinda Amani cha Umoja wa Afrika nchini Somalia AMISOM imetoa wito wa kupunguza askari wa kikosi hicho, na kukabidhi hatua kwa hatua majukumu ya ulinzi wa amani kwa Jeshi la Serikali ya Somalia.

    Katika mkutano wake uliofanyika jumanne nchini Ethiopia na kuhudhuriwa na wanadhimu wakuu wa majeshi ya ulinzi, wawakilishi kutoka nchi zilizopeleka askari wake kwenye kikosi hicho ambazo ni Burundi, Djibouti, Ethiopia, Kenya, Nigeria na Uganda, Somalia na nchi wafadhili, ilikubalika kuwa wataalam wanapaswa kuchagua njia, na pia kuandaa mpango wa kuwaondoa askari hao nchini Somalia.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako