• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Marekani yatangaza kuwawekea vikwazo maofisa wa Sudan Kusini

    (GMT+08:00) 2017-09-07 09:37:29

    Serikali ya Marekani jana imetangaza kuwawekea vikwazo maofisa waandamizi wawili wa serikali ya Sudan Kusini, ofisa mmoja wa zamani wa serikali, na kampuni tatu kutokana na kuvuruga amani, usalama na utulivu wa taifa.

    Wizara ya mambo ya nje na wizara ya fedha za Marekani zimesema kwamba vikwazo hivyo vimewekwa dhidi ya naibu waziri wa ulinzi wa Sudan Kusini Malek Reuben, waziri wa habari Michael Makuei na aliyekuwa mnadhimu mkuu wa jeshi Paul Malong, na kampuni tatu zinazomilikiwa na Reuben pia zimewekewa vikwazo.

    Taarifa iliyotolewa na wizara ya mambo ya nje ya Marekani imesema viongozi wa Sudan Kusini lazima watekeleze makubaliano yaliyosainiwa mwaka 2015 kuhusu kusitisha vita na makundi ya upinzani.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako