• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Ushirikiano kati ya nchi za BRICS una umuhimu mkubwa zaidi duniani

  (GMT+08:00) 2017-09-07 09:51:12

  Mjumbe wa taifa wa China Bw. Yang Jiechi amezungumzia mafanikio yaliyopatikana katika Mkutano wa tisa wa viongozi wa nchi za BRICS, na mazungumzo kati ya nchi zinazoibuka kiuchumi na nchi zinazoendelea duniani.

  Bw. Yang amesema wakati maendeleo ya dunia yanapokabiliwa na mabadiliko yasiyotarajiwa, mkutano huo umechangia katika kuimarisha ushirikiano kati ya nchi hizo, kutoa mapendekezo mbalimbali yenye busara na kuhimiza maendeleo ya amani na maendeleo ya dunia. Amesema anaamini kuwa ushirikiano kati ya nchi za BRICS utakuwa na ufanisi, umuhimu na msukumo mkubwa, na utapata maendeleo zaidi katika uanzishaji wa soko kubwa la biashara na uwekezaji, mzunguko wa fedha na muunganiko wa miundo mbinu.

  Bw. Yang amesema, wakati wa mkutano huo, nchi tano za BRICS zilisaini makubaliano zaidi ya 30 katika sekta mbalimbali zikiwemo uchumi, biashara, fedha na uvumbuzi.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako