• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Tanzania yashirikiana na Burundi, Zambia na DRC katika kuhifadhi Ziwa Tanganyika

  (GMT+08:00) 2017-09-07 09:51:44

  Serikali ya Tanzania jana imesema imefanya mazungumzo na Benki ya Dunia kuhusu kukusanya fedha ili kuhifadhi Ziwa Tanganyika kutokana na athari ya mabadiliko ya hali ya hewa.

  Waziri wa nchi katika ofisi ya makamu wa rais anayeshughulikia mambo ya mazingira January Makamba amesema, Tanzania inashirikiana na Burundi, Zambia na Jamhuri ya kidemokrasia ya Kongo zinazotumia ziwa hilo kwa pamoja ili kulihifadhi kutokana na maafa ya kimazingira. Amesema, Ziwa Tanganyika linakabiliwa na tishio kubwa la uchafuzi na kushuka kwa kima cha maji ambalo linasababishwa na mabadiliko ya hali ya hewa.

  Ameongeza kuwa, nchi hizo nne zimeamua kutafuta uungaji mkono wa Benki ya Dunia ili kuchangia mradi wa ujenzi wa ukuta katika mto Lukuga ambao maji yake yanatoka kwenye Ziwa hilo.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako