• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Mkutano wa viongozi wa nchi za BRICS wafikia matokeo mazuri

  (GMT+08:00) 2017-09-07 17:56:45

  Msemaji wa wizara ya biashara ya China Bw. Gao Feng amesema, kwenye mkutano wa tisa wa viongozi wa nchi za BRICS na mkutano wa nchi zinazoibuka kiuchumi na zile zinazoendelea iliyofanyika mjini Xiamen, China ilipata mafanikio. Amesema viongozi hao walisaini nyaraka nyingi za mapendekezo kuhusu ushirikiano wa kiuchumi na biashara. Viongozi wa nchi tano za BRICS walishuhudia waziri wa biashara wa China Bw. Zhong Shan na wenzake wa nchi za BRICS wakisaini mwongozo wa utekelezaji wa ushirikiano wa uchumi na biashara kati ya nchi hizo na kuanzishwa kwa mchakato mpya wa ushirikiano wa uchumi na biashara katika mwongo wa pili.

  Msemaji wa wizara ya biashara ya China Bw. Gao Feng amesema, mkutano wa viongozi wa nchi za BRICS uliofanyika mjini Xiamen ulitoa mpango kamili kwa ajili ya kuhimiza maendeleo ya biashara. Anasema,

  "La Kwanza, mkutano huo ulipitisha pendekezo la kuhimiza ushirikiano wa biashara ya kielektroniki kati ya nchi za BRICS, na kuamua kuanzisha kikundi cha watu wanaoshughulikia biashara ya kielektroniki, na kuanzisha ushirikiano wa biashara hii katika sekta mbalimbali. La pili, ulipitisha mpango wa ushirikiano wa biashara za huduma, na kuanzisha ushirikiano halisi hasa katika shughuli za utalii, elimu na afya. La tatu, ulipitisha ujenzi wa mtandao wa forodha ya kielektroniki, ili kuinua kiwango cha mawasiliano ya miundombinu na kurahisisha biashara kati ya nchi hizo. Mwisho, ulipitisha kanuni ya mwongozo ya ushirikiano wa haki miliki za kiujuzi, na kuongeza ushirikiano kati ya nchi za BRICS katika upashanaji habari kuhusu haki miliki, uratibu wa msimamo na ujenzi wa uwezo, ili kuunga mkono mfumo wa uvumbuzi na maendeleo ya uchumi wa nchi za BRICS."

  Adha, mkutano huo pia ulipitisha waraka wa mwongozo kwa ajili ya kurahisisha shughuli za uwekezaji, na kuamua njia ya kukuza ushirikiano wa uchumi na teknolojia. Pia ulifikia makubaliano muhimu kuhusu juhudi za kuunga mkono mfumo wa biashara kati ya nchi mbalimbali, na kupinga vitendo vya kujilinda kibiashara.

  Hivi karibuni idara zinazohusika zilipendekeza kufanya utafiki kuhusu ujenzi wa eneo la biashara huria kati ya nchi za BRICS, hali ambayo imefuatiliwa sana na pande mbalimbali. Bw. Gao Feng amesema, ujenzi huo unategemea nia na juhudi za pamoja za nchi zinazohusika, na China inafurahia ujenzi huo. Anasema,

  "Hadi sasa, China imesaini makubaliano ya biashara huria na nchi 23, wakati huo huo pia inasukuma mbele mazungumzo kadhaa kuhusu biashara huria. Kutoka mwanzoni ushirikiano wa uchumi na biashara ni sehemu muhimu ya ushirikiano kati ya nchi za BRICS. Tunajitahidi siku zote kujenga soko kubwa la kufungamana la nchi za BRICS."

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako