• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Vifaa vingine vya mfumo wa THAAD vyasafirishwa kwenye kituo cha Seongjugun nchini Korea Kusini

    (GMT+08:00) 2017-09-07 18:47:59

    Majeshi ya Marekani na Korea Kusini yamesafirisha magari manne ya kurusha makombora na vifaa husika vya mfumo wa ulinzi dhidi ya makombora kwenye kituo cha THAAD cha jeshi la Marekani huko Seongjugun nchini Korea Kusini.

    Wizara ya ulinzi ya Korea Kusini inasema Marekani na Korea Kusini zimemaliza mpango wa muda wa mfumo wa THAAD nchini Korea Kusini . Kuweka mfumo wa THAAD kwa ukamili kutategemea matokeo ya tathmini ya athari ya vifaa hivyo kwa mazingira .

    Msemaji wa wizara ya mambo ya nje ya China Bw. Geng Shuang amesisitiza kuwa China siku zote inaipinga kithabiti Marekani kuweka mfumo wa THAAD nchini Korea Kusini, na kusisitiza Marekani na Korea Kusini zisimamishe mara moja mchakato wote wa kupanga mfumo huo.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako