• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Mfuko wa afya wa ukanda mmoja njia moja wawasaidia watoto wa Afghanstan

  (GMT+08:00) 2017-09-07 19:20:23

  Watoto 17 kutoka Afghanistan wenye matatizo ya moyo wametibiwa na madaktari wa China mjini Urumqi mkoani Xinjiang. Watoto hao ni kati ya watoto 21 waliozaliwa na matatizo ya moyo, ambao walikuja China mwezi uliopita kwa ajili ya matibabu wakiambatana na wazazi wao.

  Gharama za usafiri na matibabu ya watoto hao pamoja na wazazi hao ziligharamiwa na mfuko wa afya wa ukanda mmoja, njia moja.

  Timu ya madaktari 11 kutoka Hospitali ya Xinjiang na watalaam kutoka hospitali mbili za hapa Beijing waliongoza upasuaji wa watoto hao 17. Watoto wengine wanne walilazimika kurudishwa nyumbani Afghanistan kutokana na hali zao kiafya kuwa na utatanishi.

  Watoto waliotibiwa na wazazi wao, wataendelea kuwepo hospitali hali yao itakapotengemaa.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako