• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Umoja wa Afrika na Umoja wa Mataifa waitisha mkutano wa amani na usalama mjini Addis Ababa

    (GMT+08:00) 2017-09-07 19:20:54

    Baraza la amani na usalama la Umoja wa Afrika na baraza la usalama la Umoja wa Mataifa yatakuwa na mkutano wa pamoja jumatatu ijayo mjini Addis Ababa, kujadili hali ya amani na usalama barani Afrika, hasa nchini Somalia, Sudan Kusini na kwenye bonde la Ziwa Chad.

    Mkutano huo umetanguliwa na majadiliano yasiyo rasmi yaliyofanyika leo, yakizingatia ushirikiano kati ya pande mbili, kugharamia shughuli za amani na usalama za Umoja wa Afrika, na ujenzi wa amani baada ya vita.

    Mkuu wa ujumbe wa Ethiopia kwenye Umoja wa Mataifa ambaye pia ni mwenyekiti wa baraza la usalama Bw. Tekeda Alemu amesema mkutano wa majadiliano utahimiza uhusiano kati ya pande mbili.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako