• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Sudan yafunga mipaka yake na Sudan Kusini, Chad na Libya ili kuzuia magendo ya silaha

    (GMT+08:00) 2017-09-07 19:20:58

    Sudan imefunga mipaka yake na Sudan Kusini, Chad na Libya kuzuia magendo ya silaha.

    Makamu wa rais wa Sudan Bw. Hassabo Abdul-Rahman amehutubia mkutano wa wanafunzi huko Khartoum akisema, mipaka na Libya, Chad na Sudan Kusini imefungwa ili kuzuia magendo ya silaha na magari.

    Bw. Abdul-Rahman ameongeza kuwa katika kipindi kilichopita, magari elfu 60 hivi yamesafarishwa kimagendo kuingia Sudan kutoka Libya, Chad na Sudan Kusini ambako baadhi ya magari hayo yanatumiwa kwenye uhalifu ikiwemo mauaji, magendo, kutakatisha pesa na dawa za kulevya.

    Ameeleza zaidi kuwa polisi wa kimataifa hivi karibuni imetuma matakwa kwa Sudan kusajili data za magari hayo ya magendo ili kusaidia kutambua mitandao ya uhalifu inayohusika na vitendo vya kihalifu.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako