Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa limetoa taarifa kulaani vikali shambulizi dhidi ya ujumbe wa Umoja wa Mataifa nchini Mali, ambalo limesababisha vifo vya walinzi wawili wa amani kutoka Chad na wengine wawili kujeruhiwa katika sehemu ya Kidal nchini Mali.
Taarifa hiyo imesema, wajumbe wa baraza hilo wanatoa salamu za rambirambi kwa jamaa wa walinzi waliouawa, serikali ya Chad na ujumbe huo, kuwatakia majeruhi wapone haraka na kutoa heshima kwa walinzi wa amani walio hatarini nchini Mali.
Taarifa hiyo pia imesema, wajumbe wa baraza hilo wanaitaka serikali ya Mali kufanya uchunguzi kuhusu shambulizi hilo na kuwakamata washambuliaji.
© China Radio International.CRI. All Rights Reserved. 16A Shijingshan Road, Beijing, China. 100040 |