• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Ubalozi wa China nchini Somalia wafanya shughuli ya kuwaaga wanafunzi watakaosoma nchini China

    (GMT+08:00) 2017-09-07 19:22:56

    Ubalozi wa China nchini Somalia umefanya shughuli ya kuwaaga wanafunzi wa nchi hiyo waliopata udhamini wa masomo wa serikali ya China kuja kusoma nchini China.

    Balozi wa China nchini humo Bw. Tan Jian na waziri wa elimu wa Somalia Bw. Dahir Osman wamehudhuria na kutoa hotuba katika shughuli hiyo. Maofisa wa serikali ya Somalia na wajumbe wa wanafunzi wa Mogadishu na wazazi wao pia wameshiriki kwenye shughuli hiyo.

    Mwaka huu wanafunzi 42 wa Somali wamepata udhamini wa masomo wa serikali ya China. Bw. Tan amesema urafiki kati ya China na Somalia una historia ndefu, vijana ni mustakbali wa maendeleo ya uhusiano kati ya nchi hizo mbili, na elimu ni sekta muhimu ya ushirikiano kati ya nchi hizo mbili. Amezitaka nchi hizo kuendelea kuimarisha mawasiliano na ushirikiano, na kufanya mawasiliano kati kizazi cha vijana.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako