• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Mechi kati ya Afrika Kusini na Senegal kurudiwa tena Novemba

  (GMT+08:00) 2017-09-08 08:48:56

  Mechi ya kufuzu kombe la dunia kati ya Afrika Kusini na Senegal itarudiwa tena baada ya refa aliyesimamiwa mechi hiyo kupigwa marufuku na Fifa.

  Refa huyo raia wa Ghana Joseph Lamptey, alipiwa marufuku kwa kusimamia mechi kwa njia isiyofaa.

  Aliwapa penalti Afrika Kusini ambao walishinda kwa mabao 2-1 mwezi Novemba mwaka uliopita kwa kunawa mpira lakini kanda ya video baaadaye ilionyesha kuwa mpira huo ulimgonga kwenye goti mlinzi wa Senegal Kalidou Koulibaly. Mechi hiyo itachezwa tena Novemba mwaka huu.

  Lamptey, ambaye pia alisimamia mechi katika mashindano ya Olimpki huko Rio mwaka uliopita alipigwa marufuku ya maisha mwezi Machi lakini juzi Jumatano marufuku hiyo ilibatiliswa na mahakama ya michezo. Senegal na Afrika Kusini kwa saa wako nafasi ya tatu na nne mtawalia katika kundi lao D nyuma ya Burkina Faso na Cape Verde.

  Ni timu moja pekee ya kwanza katika kundi ambayo itafuzua kwa mechi za kombe la dunia nchini Urusi mwaka ujao.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako