• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Duru ya pili ya kuwania tiketi za kufuzu kombe la dunia nchini Urusi kuendelea tena Oktoba

  (GMT+08:00) 2017-09-08 08:55:09

  Duru ya pili ya makundi ya kuwania tiketi za kufuzu kushiriki kombe la dunia hapo mwakani nchini Urusi inatarajiwa kuendelea tena mwezi Octoba wakati kwa upande wa Afrika vitakali itakuwa ni mchezo kati ya timu ya taifa ya Cameroon itakayo wavaa wa Algeria. Mchezo wa Cameroon dhidi ya Algeria unatarajiwa kupigwa Octoba 7 wakati ambapo michezo mingine ikichezwa katika viwanja tofauti barani Afrika.

  Timu ya taifa ya Guinea ikijitupa uwanjani kuvaana na Tunisia wakati Libya itacheza na DR Kongo wakati siku hiyo ya tarehe 7 ya mwezi Octoba Nigeria ikiwa uwanjani dhidi ya Zambia.

  Michezo mingine itakayopigwa mapema kwa Afrika ni Octoba 6, wakiwa Mali dhidi ya Ivori Coast, Morocco na Gabon, Afrika Kusini dhidi ya Burkinafaso huku Caper Verde ikicheza na Senegal.

  Sweeden itaikabili Luxermburg, Austria watachuana na Serbia, Uturuki dhidi ya Iceland, Italia itakutana na Macedonia, Hispania dhidi ya Albania, Montenegro na Dernmark, Moldova dhidi ya Wels, Ujerumani na Ireland ya Kaskazini na Uingereza watakutana na Slovenia.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako