• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Wanawake wanne wa Marekani wafuzu kuingia nusu fainali Us Open

  (GMT+08:00) 2017-09-08 08:56:45

  Mcheza tenis, Madison Keys amefanikiwa kuingia hatua ya nusu fainali ya michuano ya wazi ya Marekani 'US Open' baada ya kumtoa, Kaia Kanepi na hivyo kuifanya Marekani kuingiza wanawake wanne hatua ya nusu fainali. Keys mwenye umri wa miaka 22, ametinga hatua hiyo baada ya ushindi wa jumla ya seti 6-3 6-3 na kuungana na wamarekani wenzake wanadada, Coco Vandeweghe, Venus Williams na Sloane Stephens ambao tayari wametinga hatua hiyo.

  Hii ni mara ya kwanza tangu mwaka 1981 kwa Marekani kuingiza wanawake wanne kwa pamoja katika hatua ya nusu fainali ya US Open na kwa mara ya kwanza katika mashindano mengine tangu walivyofanya hivyo Wimbledon mwaka 1985.

  Baada ya ushindi huo, Madison Keys anayeshika nafasi ya 16 katika viwango vya ubora wa mchezo huo ulimwenguni amesema kuwa amefurahishwa na matokeo aliyoyapata.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako