• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Upigaji kura kuhusu kufanya sheria za Umoja wa Ulaya kuwa sheria za Uingereza sio kufuta sheria za Uingereza

    (GMT+08:00) 2017-09-08 09:20:06

    Waziri anayeshughulikia mambo ya Uingereza kujitoa Umoja wa Ulaya Bw David Davis ameliambia bunge la Uingereza uamuzi wa kuzipigia kura sheria za umoja wa Ulaya, hauna maana ya kufuta sheria hizo.

    Wabunge wa Uingereza wanaanza mjadala wa siku tatu kuhusu mswada unaotaka kufanya sheria za muda wa miaka 40 za umoja wa Ulaya kuwa sheria za Uingereza itakapofika mwezi Machi mwaka kesho, wakati ambapo uanachama wa Uingereza kwenye Umoja wa Ulaya utakoma.

    Bw Davis amewaomba wabunge wa vyama vyote kushirikiana naye kutunga sheria itakayohakikisha kuwa sheria za Uingereza zinaanza kufanya kazi mara moja baada ya Uingereza kujitoa Umoja wa Ulaya.

    Hata hivyo chama cha Leba kimewaagiza wanachama wake kuukataa muswada huo.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako