• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Hali ya kukwama kisiasa yatishia kukwamisha upigaji kura Kenya kwenye uchaguzi mpya Kenya

    (GMT+08:00) 2017-09-08 09:20:28

    Kauli zinazoendelea kutolewa na wadau wakubwa wa uchaguzi mkuu wa Kenya uliopangwa kufanyika Oktoba 17 zinatishia kukwamisha uchaguzi huo.

    Mvutano mkubwa upo kati ya wagombea wanaotarajiwa kukutana kwenye uchaguzi huo kuhusu tarehe ya uchaguzi. Muungano wa Jubilee unaoongozwa na Rais Uhuru Kenyatta umeridhia tarehe ya uchaguzi, na muungano wa NASA unaoongozwa na Bw Raila Odinga unapinga tarehe hiyo.

    Tume ya uchaguzi ya Kenya inapanga kukutana na pande mbili ili kujadili tofauti hizo na kutafuta ufumbuzi.

    Wakati huo huo mabalozi 12 kutoka nchi za magharibi wametoa mwito kwa wakenya kuepuka vurugu siku kabla ya uchaguzi huo. Mabalozi hao wamezitaka idara za usalama za Kenya kutotumia mabavu kupita kiasi na kulinda maisha na mali za watu.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako