• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Sudan Kusini yasema vikwazo ilivyowekewa na Marikani vitaharibu juhudi za amani

    (GMT+08:00) 2017-09-08 09:33:57

    Serikali ya Sudan Kusini imesema vikwazo vilivyowekwa na Marekani dhidi ya maofisa watatu wa serikali ya Sudan Kusini vitaharibu juhudi na mchakato wa amani nchini humo.

    Msemaji wa wizara ya mambo ya nje wa Sudan Kusini Bw Mawien Makol amesema wizara ya fedha ya Marekani Juamtano ilitangaza kuwawekea vikwazo maofisa watatu wa Sudan Kusini kutokana na kuvuruga amani na usalama wa taifa.

    Bw Makol ameongeza kuwa vikwazo hivyo vitaharibu juhudi zinazoendelea kufanyika kwa ajili ya amani, na kumaanisha serikali ya Marekani haiamini serikali ya Sudan Kusini, na imeweka vikwazo hivyo wakati serikali ya Sudan Kusini inafanya juhudi kubwa kwenye mchakato wa amani nchini humo.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako