• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Semina ya kimataifa kuhusu ushirikiano China na Afrika na maendeleo ya Afrika yafunguliwa Malawi

    (GMT+08:00) 2017-09-08 09:58:08

    Semina ya kimataifa kuhusu ushirikiano kati ya China na Afrika na maendeleo ya Afrika imefunguliwa jana huko Lilongwe, mji mkuu wa Malawi. Semina hiyo inaendeshwa na ubalozi wa China nchini Malawi na wizara ya mambo ya nje na ushirikiano wa kimataifa wa Malawi.

    Balozi wa China nchini Malawi Bw. Wang Shiting amesema, semina hiyo inalenga nchi zenye ukubwa wa kati na ndogo barani Afrika, na kwamba China inapenda kuzipatia nchi hizo uzoefu wa kujiendeleza, kutoa uungaji mkono wa kifedha na kukuza biashara za kunufaishana na nchi hizo.

    Waziri wa mambo ya nje na ushirikiano wa kimataifa wa Malawi Bw. Emmanuel Fabiano amesema, kupitia semina hiyo wasomi kutoka nchi mbalimbali za Afrika wanaweza kubadilishana uzoefu, ili kuweza kunufaika zaidi kutokana na uhusiano na ushirikiano wa kibiashara kati ya nchi za Afrika na China na hivyo kutimiza maendeleo.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako