• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Njia zaidi za usafiri wa chini ya ardhi zaongezeka katika miji midogo nchini China

  (GMT+08:00) 2017-09-08 17:59:15

  Miji mingi nchini China inapanga kuwa na njia za usafiri za chini ya ardhi kwa lengo la kupunguza msongamano wa magari.

  Wizara ya Nyumba na Maendeleo ya Miji na Vijiji imesema, mpaka kufikia mwisho wa mwaka jana, jumla ya miji 30 ilikuwa na mfumo wa usafiri wa treni za chini ya ardhi, ikiwa ni ongezeko la asilimia 16.8 ikilinganishwa na mwaka 2015.

  Tangu mwezi Juni mwaka huu, mji wa Shijiazhuang mkoani Hebei, umezindua njia mbili za treni ya chini ya ardhi, ambapo jumla ya watu laki mbili wanatumia usafiri huo kila siku.

  Wataalam wanakadiria kuwa, mpaka kufikia mwaka 2020, miji 50 nchini China itakuwa na usafiri wa treni ya chini ya ardhi, na uwekezaji wake unakadiriwa kuzidi yuan trilioni 4 sawa na dola za kimarekani bilioni 615.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako