• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Mawaziri wa mambo ya nje wa China na Pakistan wafanya mazungumzo

  (GMT+08:00) 2017-09-08 18:55:23

  Waziri wa mambo ya nje wa China Bw. Wang Yi leo hapa Beijing amezungumza na mwenzake wa Pakistan Bw. Khawaja Asif ambaye yupo ziarani nchini China, na kukutana na waandishi wa habari kwa pamoja.

  Kwenye mkutano na waandishi wa habari, waziri wa mambo ya nje wa China Bw. Wang Yi amesema China na Pakistan zitakuza zaidi uhusiano wa wenzi na ushirikiano wa kimkakati kati yao. Ingawa hali ya kimataifa na kikanda imekuwa na mabadiliko makubwa, huku hali ya nchi hizo mbili zikibadilika, lakini uhusiano mzuri kati ya China na Pakistan haubadiliki, na ni nguzo imara ya kulinda amani ya kikanda. Bw. Asif pia ameusifu uhusiano huo, anasema,

  "Uhusiano kati ya Pakistan na China una historia ndefu, umethibitishwa na wakati. Uhusiano huo bado unaendelea, na ni mfano wa kuigwa na nchi nyingine. Tumejenga uhusiano huo kwa kufuata kanuni ya uaminifu, usawa na kutoingiliana mambo ya ndani. Tuna malengo ya pamoja, na kufanya ushirikiano halisi katika sekta nyingi, hali ambayo imeimarisha zaidi uhusiano kati yetu."

  Rais Donald Trump wa Marekani hivi karibuni alitangaza mkakati mpya wa nchi yake kuhusu suala la Afghanistan, akiilaani Pakistan kuhifadhi makundi ya kigaidi likiwemo kundi la Taliban. Maneno yake yamelalamikiwa na pande mbalimbali za Pakistan. Bw. Wang Yi anasema,

  "Pakistan ni ndugu na rafiki mkubwa wa China. Duniani hakuna nchi nyingine inayoelewa Pakistan kama China. Katika miaka mingi iliyopita, serikali na wananchi wa Pakistan wamechangia na kujitoa mhanga kwa juhudi za kupambana na ugaidi. Hali hii ni dhahiri, na inapaswa kuheshimiwa na jumuiya ya kimataifa."

  Baada ya Marekani kutangaza sera mpya kuhusu suala la Afghanistan, kutafuta njia mwafaka ya kisiasa ya kutatua suala hilo, ni moja kati ya malengo ya ziara ya Bw. Asif. Bw. Wang Yi amesema amefikia makubaliano mengi na Bw. Asif kuhusu suala hilo. Anasema,

  "Tumefuatilia serikali ya Marekani kutoa sera mpya kuhusu masuala ya Afghanistan na Asia ya kusini, tunatumai sera hizo zitasaidia kutimiza utulivu na amani ya kudumu ya kikanda, na pia kuzingatia ufuatiliaji wa nchi nyingine za kikanda kuhusu suala la usalama. Tunasisitiza kuwa njia pekee ya kutatua suala la Afghanistan ni kusukuma mbele mchakato wa amani na maafikiano unaoongozwa na watu wa nchi hii. China na Pakistan zitaendelea na kazi ya kiujenzi kwa ajili ya kuhimiza mchakato wa maafikiao ya kisiasa nchini Afghanistan"

  Hivi sasa uhusiano kati ya Pakistan na Afghanistan unakabiliwa na changamoto. Ikiwa rafiki na jirani mwema wa nchi hizo, China inafanya usuluhishi kutoka mwanzoni. Mwezi Juni mwaka huu, Bw. Wang Yi alitembelea nchi hizo mbili, ili kuhimiza kuboresha uhusiano kati yao na mchakato wa amani nchini Afghanistan. Kwenye mkutano na waandishi wa habari uliofanyika leo, Bw. Wang Yi amedokeza kuwa, mkutano kati ya mawaziri wa China, Pakistan na Afghanistan utafanyika ndani ya mwaka huu, ili kubadilishana maoni kuhusu masuala ya mikakati, usalama na ushirikiano, na hatimaye kujenga jukwaa jipya la ushirikiano wa kikanda. Bw. Wang Yi anaamini kuwa kutokana na jitihada za pamoja za Pakistan na Afghanistan pamoja na uungaji mkono wa China, uhusiano kati ya Pakistan na Afghanistan na ushirikiano kati ya China na nchi hizo mbili utakuwa na mustakabali mzuri.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako