• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Mvutano kati ya rais wa Zimbabwe na chama cha ANC cha Afrika Kusini waongezeka

    (GMT+08:00) 2017-09-08 18:59:32

    Mvutano kati ya Rais Robert Mugabe wa Zimbabwe na chama cha ANC cha Afrika Kusini umeongezeka baada ya rais huyo kusema kuwa hisia alizoonyesha katibu mkuu wa ANC Gwede Mantashe kuhusu kauli hasi alizotoa rais Mugabe dhidi ya mwanasiasa mashururi Hayati Nelson Mandela ni ya kijinga.

    Katika matukio mawili tofauti, rais Mugabe aliwaambia wafuasi wa chama chake cha ZANU PF kuwa Hayati Mandela alijadiliana tu ili kuondolewa gerezani na sio kwa uwezeshaji wa kiuchumi kwa watu weusi ambao wanaendelea kuteseka katika umasikini wakati watu weupe wanatajirika.

    Wiki hii, Mantashe aliwasiliana na katibu wa idara ya uongozi ya ZANU PF Ignatius Chombo na kumtaka amzuie rais Mugabe kumtukana Mandela. Hata hivyo, rais Mugabe alijibu kauli hiyo na kusema kuwa kitendo cha Mantashe ni cha kijinga, na kwamba watu ambao waliwakandamiza wazawa wa Afrika Kusini bado wanadhibiti maliasili za nchi hiyo.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako