• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Qatar yatakiwa kutekeleza matakwa 13 bila ya masharti yoyote

    (GMT+08:00) 2017-09-08 19:35:41

    Nchi nne za Saudi Arabia, Misri, Falme za Kiarabu na Bahrain zimetoa taarifa ya pamoja zikisisitiza kuwa Qatar inatakiwa kutekeleza matakwa 13 bila ya sharti lolote.

    Taarifa hiyo imetolewa baada ya Emir wa Kuwait Sabah Al-Ahmed kutoa hotuba kuhusu Qatar iko tayari kupokea matakwa 13. Emir Sabah ambaye yuko ziarani nchini Marekani amesema, kutokana na upatanishi wake, Qatar imesema iko tayari kukubali na kufanya mazungumzo ya utekelezaji wa matakwa hayo 13. Pia amesema, upatanishi wake umefanikiwa kuepusha kutatua mgogoro wa Qatar kwa njia ya kijeshi.

    Taarifa hiyo pia imesema, baada ya hotuba ya Sabah, waziri wa mambo ya nje wa Qatar Sheikh Mohammed amejibu kuwa nchi hizo nne zinatakiwa kuondoa vikwazo kwanza.

    Taarifa hiyo pia imesisitiza kuwa Qatar haiwezi kuweka sharti kabla ya kutekeleza matakwa hayo.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako