• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Rais wa Ufaransa auhimiza Umoja wa Ulaya kufanya mageuzi

    (GMT+08:00) 2017-09-08 19:35:59

    Rais Emmanuel Macron wa Ufaransa ambaye yuko ziarani nchini Ugiriki amesema, Umoja wa Ulaya unahitaji mageuzi ya kimsingi, ama sivyo utakabiliwa na hatari ya kuvunjika.

    Rais Macron amesema hayo alipotoa hotuba kwa njia ya televisheni nchini Ugiriki. Pia amesema, atatoa mpango wa Ufaransa wa kujenga upya Umoja wa Ulaya hivi karibuni, na katika miezi kadhaa ijayo, pande mbalimbali zinatakiwa kufanya mazungumzo kuhusu mageuzi.

    Waziri mkuu wa Ugiriki Bw. Alexis Tsipras pia amesema, Umoja wa Ulaya unatakiwa kuhimiza mazungumzo hayo na kujenga makubaliano mapya kuhusu demokrasia, usawa na umoja kupitia njia ya kidiplomasia. Ameongeza kuwa Umoja wa Ulaya unahitaji mageuzi ya kasi na yenye kina.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako