• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Wanasayansi wa China wazisaidia nchi za Afrika kukabiliana na mabadiliko ya hali ya hewa

    (GMT+08:00) 2017-09-08 19:36:18

    Wanasayansi 60 kutoka China na Afrika wamefanya semina yenye kaulimbiu ya "Mabadiliko ya Hali ya Hewa, Mfumo wa Kiasili na Maisha ya watu" katika ofisi za Shirika la Mpango wa Mazingira la Umoja wa Mataifa UNEP huko Nairobi, Kenya.

    Naibu mkurugenzi mtendaji wa shirika hilo Bw. Ibrahim Thiaw amesema, China ina teknolojia ya juu, vifaa vya kisasa na uzoefu katika kukabiliana na mabadiliko ya hali ya hewa, na inaweza kutoa msaada mkubwa kwa nchi za Afrika kupitia kubadilishana uzoefu na teknolojia katika sekta hiyo.

    Mkuu wa idara ya ushirikiano wa kimataifa ya taasisi ya sayansi na teknolojia ya China Bw. Cao Jinghua amesema, ushirikiano kati ya China na Afrika katika kukabiliana na mabadiliko ya hali ya hewa sio tu uko katika upande wa ushirikiano wa utafiti, bali pia unahusisha ujenzi wa uwezo, kwa mfumo kuandaa wanasayansi vijana wa Afrika.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako