• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Dar es Salaam- Wanawake wenye ulemavu nchini Tanzania wamezitaka taasisi za fedha kuwaamini na kupunguza riba kwenye mikopo wanayotoa ili waweze kukopa.

  (GMT+08:00) 2017-09-08 20:55:08
  Wanawake wenye ulemavu nchini Tanzania wamezitaka taasisi za fedha kuwaamini na kupunguza riba kwenye mikopo wanayotoa ili waweze kukopa. Kauli hiyo inakuja wakati ambapo utafiti unaonesha kuwa walemavu wengi hawako karibu na taasisi za fedha jambo ambalo linafanya wanyimwe fedha kwa kudhaniwa kuwa hawana uwezo wa kulipa licha ya kujishughulisha na shughuli mbali mbali za kiuchumi. Mwenyekiti wa jumuia la wanawake walemavu nchini humo Bibi Doris Kulanga amesema hakuna njia nyingine ya kuwasaidia wanawake isipokuwa kuwapatia mikopo yenye riba nafuu.

  Wanawake wengi walemavu barani Afrika kwa muda mrefu wamekuwa wakisahaulika kitendo ambacho kimewafanya waendelee kuwa masikini.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako