• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Mpango uliotolewa na Russia na China ni mpango mzuri zaidi wa kutatua suala la peninsula ya Korea

    (GMT+08:00) 2017-09-09 18:22:55

    Msemaji wa wizara ya mambo ya nje ya Russia Bibi Maria Zakharova amesema hivi sasa mpango uliotolewa na Russia na China ni mpango mzuri zaidi wa kutatua suala la peninsula ya Korea.

    Msemaji huyo amesema hivi karibuni Korea Kaskazini ilifanya tena majaribio ya nyuklia, na kuifanya hali ya peninsula ya Korea izidi kuwa mbaya.

    Amesema kuiwekea vikwazo Korea Kaskazini kadri iwezavyo kutasababisha mgogoro wa kijeshi au janga la kibinadamu katika Asia ya Kaskazini Mashariki. Pande husika zinatakiwa kufanya juhudi kwa pamoja na kutafuta njia ya kutatua suala hilo kwa amani. Hivi sasa Russia haijagundua mpango mzuri zaidi kuliko ule uliotolewa na Russia na China, na inawakaribisha watu kutoa mapendekezo mapya kuhusu mpango huo.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako