• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Wizara ya mawasiliano ya simu ya Nigeria na kampuni ya Huawei zaanzisha mradi wa "mbegu kwa siku zijazo"

  (GMT+08:00) 2017-09-10 18:04:14

  Wizara ya mawasiliano ya simu ya Nigeria na kampuni ya Huawei zimefanya hafla ya kuzindua mradi wa "mbegu kwa siku zijazo". Wanafunzi kumi hodari kutoka Nigeria watapata mafunzo ya wiki mbili nchini China kuanzia tarehe 9.

  Habari zinasema kampuni ya Huawei na serikali ya Nigeria zilisaini mkataba wa ushirikiano mwezi Oktoba mwaka 2015, ambao umeamua kuwa kampuni hiyo itatoa mafunzo kwa wanafunzi 2000 wa Nigeria, na kutuma baadhi ya wanafunzi hodari kwenda China kupata mafunzo. Hivi sasa wanafunzi 1345 wamepata mafunzo kuhusu mawasiliano ya simu, mawimbi aina ya micro na utengenezaji wa simu za mkononi katika vituo vya mafunzo mjini Abuja na Lagos.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako