• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Mashirika yasiyo ya kiserikali yamekuwa nguvu muhimu ya kuzuia ardhi isibadilike kuwa jangwa nchini China

  (GMT+08:00) 2017-09-10 18:04:29

  Kwenye mkutano wa mashirika yasiyo ya kiserikali yanayoshughulikia kazi ya kuzuia ardhi isibadilike kuwa jangwa uliofanyika jana, naibu mkurugenzi wa idara ya misitu ya China Bw. Liu Dongsheng amesema, katika miaka ya hivi karibuni, mashirika mengi yasiyo ya kiserikali yamekuwa nguvu muhimu ya kudhibiti kuenea kwa jangwa nchini China.

  Eneo la jangwa nchini China limekuwa linaendelea kupungua katika miaka zaidi ya 10 tangu mwaka 2004. Bw. Liu amesema mashirika hayo ni daraja kati ya serikali na jamii, China inatilia mkazo kuwahamasisha watu mbalimbali kwenye jamii kushiriki kwenye kazi ya kudhibiti kuenea kwa jangwa na kutoa mapendekezo kwa serikali kuhusu utungaji wa sera husika, pia imekuwa inaendelea kuimarisha mawasiliano na ushirikiano na nchi husika, mashirika ya kimataifa na mashirika yasiyo ya kiserikali kutoka nchi mbalimbali, ili kuingiza mitaji, teknolojia na mawazo ya kisasa kwa kazi ya kudhibiti kuenea kwa jangwa.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako