• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Makamu rais wa Iran asisitiza kuendelea kufuata makubaliano ya suala la nyuklia la Iran

    (GMT+08:00) 2017-09-10 18:04:30

    Makamu rais wa Iran Ali Akabar Salehi ambaye pia ni mwenyekiti wa Shirika la Nishati ya Atomiki la Kimataifa(IAEA) amesema, Iran itafuata makubaliano ya suala la nyuklia la Iran hata kama Marekani ikijitoa kwenye makubaliano hayo lakini nchi nyingine husika zikiendelea kuyafuata.

    Bw. Salehi amesema, vikwazo vya Marekani dhidi ya Iran vinalenga kuweka hali mbaya kwa biashara ya Iran na kuzuia ushirikiano kati ya Iran na makampuni na benki kuu za kimataifa.

    Habari zinasema, rais Donald Trump wa Marekani ameendelea kutoa vikwazo dhidi ya Iran. Ingawa mpango wake wa kujitoa kwenye makubaliano hayo umezuiliwa na waziri wa mambo ya nje na wa ulinzi wa Marekani, lakini kitendo chake kimeleta wasiwasi kwa makampuni ya magharibi yanayopanga kuwekeza nchini Iran.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako