• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Jeshi la Syria lavunja hali ya kuzingirwa kwa uwanja wa ndege wa Deir al- Zour na kundi la IS

    (GMT+08:00) 2017-09-10 18:17:08

    Shirika la habari la Syria SANA limeripoti kuwa jeshi la Syria siku ya Jumamosi lilivunja hali ya kuzingirwa kwa uwanja wa ndege wa kijeshi wa Deir al-Zour mji wa mashariki mwa Syria na kundi la Islamic State (IS).

    Tukio hilo lilikuja baada ya askari waliokuwa wakisonga mbele kuelekea kwenye uwanja wa ndege, ambao ulikuwa umezingirwa na IS pamoja na mji huo kwa miaka mitatu.

    Wizara ya mambo ya nje ya Syria imesema kuwa vita inakaribia kuisha baada ya kundi la kigaidi la IS kupigwa vibaya.

    Mapema juma hili, jeshi la Syria na askari washirika wa Russia walizingira kambi hiyo ya IS kupitia brigedi namba 137 iliyoko upande wa magharibi mwa jiji.

    Serikali ya Syria imetuma chakula na dawa kwa raia 93,000 waliozingirwa mjini humo kwa miaka kadhaa.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako