• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Polisi nchini Misri wamewaua magaidi 9 mkoani Giza

    (GMT+08:00) 2017-09-10 19:20:51

    Jumla ya magaidi 9 wameuawa na polisi watano kujeruhiwa siku ya Jumapili wakati polisi walipofanya mashambulizi ya ghafla katika mkoa wa Giza karibu na mji mkuu wa Cairo.

    Ofisa wa usalama ameliambia shirika la habari la nchi hiyo MENA kuwa, magaidi hao walikuwa wamejificha katika nyumba mbili kwenye mtaa mmoja katika wilaya ya Agouza mkoani humo wakijiandaa kufanya shughuli kadhaa za ugaidi.

    Ofisa huyu amesema polisi walipokaribia nyumba hizo, magaidi hao walianza kuwafyatulia risasi polisi kutoka moja ya nyumba hizo, na mgaidi kutoka nyumba nyingine alilipua bomu.

    Ofisa huyu ameongeza kuwa, polisi wamekamata silaha, mabomu na nyaraka zinazohusiana na ugaidi kwenye shambulizi hilo.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako