• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • KCB, Kabras Sugar zafuzu robo fainali –Kabeberi Sevens

  (GMT+08:00) 2017-09-11 08:50:39

  Miamba ya raga za wachezaji 7 kila upande Homeboyz, KCB na Kabras Sugar wametinga robo-fainali ya duru ya pili ya Raga za Kitaifa ya Kabeberi Sevens bila kushindwa jijini Nairobi. Klabu za Oilers, Strathmore Leos, Kenya Harlequins, Nondies na Impala Saracens zilinasa tiketi baada ya kushinda mechi zao mbili za kwanza.

  Mbio za magari za Rwanda Mountain: Manvir Sigh ashinda

  Mashindano ya mbio za magari ya Rwanda mountain Rally yamemalizika nchini Rwanda huku dereva kutoka Kenya Manvir Singh akiibuka mshindi.

  Manvir akiendesha gari lake aina ya skoda ameshinda awamu zote zilizochezwa na kunyakua ubingwa wa mashindano hayo. Manvir akiwa na msaidizi wake walitumia saa 1:47:06, nafasi ya pili ilikamatwa na Giancarlo Davite pamoja na msaidizi wake waliotumia saa 1:51:40 huku Bukera Valery pamoja na Khetia Nital wakimaliza kwa saa 1:59:02 mashindano hayo yalianza Ijumaa yalishirikisha washindani 16.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako