• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Serikali ya Sudan yasema iko tayari kufanya mazungumzo na kundi la SPLM kaskazini

    (GMT+08:00) 2017-09-11 09:27:50

    Serikali ya Sudan imesema iko tayari kufanya mazungumzo tena na waasi wa SPLM tawi la kaskazini kuhusu maeneo ya Kordofan Kusini na Blue Nile.

    Mjumbe wa upande wa serikali kwenye mazungumzo hayo Bw Abdul-Rahman Abu-Median amesema ujumbe wa serikali uko tayari kwa kufuata mapendekezo yaliyotolewa na wapatanishi wa Umoja wa Afrika.

    Kauli hiyo ya serikali ya Sudan inafuatia juhudi za ujumbe wa ngazi ya juu wa Umoja wa Afrika, ambao mwezi Agosti ulifanya majadiliano na kundi la SPLM tawi la kaskazini kuhusu kurudisha mazungumzo ya amani.

    Kundi la SPLM Tawi la kaskazini limekuwa kwenye mgawanyo wa ndani, ambao mwezi Julai ulisababisha kuondolewa kwa kiongozi wake Malik Agar na nafasi yake kuchukuliwa na makamu wake Bw Abdel Aziz Hilu.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako