• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Sudan yautaka Umoja wa Ulaya usaidie kuondoa vikwazo vya Marekani

    (GMT+08:00) 2017-09-11 09:28:15

    Serikali ya Sudan imezitaka nchi za umoja wa Ulaya kufanya kazi ya kusaidia kuondoa vikwazo vilivyowekwa na serikali ya Marekani dhidi ya Sudan mwezi Oktoba kama ilivyopangwa.

    Waziri wa mambo ya nje wa Sudan Bw Ibrahim Ghandour amekutana na kiongozi wa ujumbe wa Umoja wa Ulaya nchini Sudan, pamoja na mabalozi wa baadhi ya nchi za Ulaya. Amewaambia mabalozi hao kuwa ni lengo la pamoja kuhakikisha vikwazo vya Marekani dhidi ya Sudan vinaondolewa kikamilifu mwezi Oktoba kama ilivyopangwa. Amesema kuondolewa kwa vikwazo hivyo kutafungua njia ya ushirikiano wa kiuchumi na kibiashara kati ya Sudan na Umoja wa Ulaya, na nchi nyingine duniani.

    Mwezi Julai Marekani ilirefusha kwa miezi mitatu muda wa kuamua kama iondoe vikwazo dhidi ya Sudan, kufuatia rekodi yake ya haki za binadamu na mambo mengine.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako