• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Wawili wauawa katika shambulizi la kujitoa mhanga Somalia

    (GMT+08:00) 2017-09-11 09:32:30

    Shambulizi la mlipuko wa kujitoa mhanga limetokea jana katikati mwa Somalia, na kusababisha vifo vya watu wasiopungua wawili, na wengine 15 kujeruhiwa wakiwemo wanahabari watatu.

    Gavana wa jimbo la Hiiran Bw Omar Adan Ibrahim amethibitisha vifo vya watu wawili katika shambulizi hilo, na kusema uchunguzi umeanza. Amesema mshambuliaji wa kujitoa mhanga alijilipua kwenye duka moja maarufu lililoko karibu na kituo cha kijeshi cha Djibouti jimboni Hiiran.

    Magaidi wa Kundi la Al-Shabaab wanaopambana na serikali wametangaza kuhusika na shambulizi hilo ambalo limetokea wakati kundi hilo limeongeza mashambulizi.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako