• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Kenya na Tanzania zaamua kuthibitisha bidhaa ili kukomesha masuala ya kibiashara

    (GMT+08:00) 2017-09-11 10:11:36

    Kenya na Tanzania zimekubaliana kufanya zoezi la pamoja la kuthibitisha bidhaa zote zinazoagizwa na kusafirishwa kati yao ili kusaidia kutatua masuala ya kibiashara kati ya nchi hizo mbili.

    Kwa mujibu wa taarifa ya pamoja iliyotolewa na katibu mkuu wa biashara wa Kenya Chris Kiptoo na mwenzake wa Tanzania Adolf Mugenda mjini Nairobi, zoezi hilo likianza, bidhaa zinazotengenezwa nje ya eneo la kuzalisha bidhaa kwa ajili ya uuzaji nje kama vile mafuta, mafuta ya kupikia, saruji, vitambaa hazitazuiliwa na nchi hizo mbili.

    Taarifa hiyo iliyotolewa baada ya mazungumzo ya siku tatu, inasema pande hizo mbili zimekubaliana kufanya mazungumzo kila baada ya muda, kujadili masuala yanayofuatiliwa kwa pamoja na fursa zitakazohimiza biashara za kunufaishana kati ya nchi hizo mbili.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako