• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Merkel asema nchi za EU zinazokataa mpango wa kupokea wakimbizi hazitapewa msaada katika masuala mengine

    (GMT+08:00) 2017-09-11 10:14:35

    Gazeti la Ujerumani FAZ limesema chansela wa nchi hiyo Bibi Angela Merkel ameonya kuwa, nchi wanachama wa Umoja wa Ulaya zinazokataa kufuata mpango wa Umoja huo kuhusu kupokea wakimbizi hazitapewa misaada katika masuala mengine.

    Bibi Merkel amesema endapo Umoja wa Ulaya hautakuwa na mshikamano katika suala la wakimbizi, basi pia utashindwa kuwa na umoja katika masuala mengine.

    Amesema kama Umoja wa Ulaya ukiweka sera imara zaidi kuhusu suala la wakimbizi, itakuwa rahisi zaidi kutekeleza mpango wa kuchangia kupokea wakimbizi.

    Pia amesema hali ya kutokuwa na imani na wahamiaji halali itaondolewa endapo suala la wakimbizi litaweza kutatuliwa kwa mafanikio, ambapo mipaka ya Umoja wa Ulaya italindwa vizuri na ushirikiano wa kusaidia maendeleo ya nchi za Afrika utaleta ufanisi wa kuzuia uhamiaji haramu wa kwenda Ulaya.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako