• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Rais Xi Jinping apongeza mkutano wa 22 wa shirika la waendesha mashitaka la kimataifa

  (GMT+08:00) 2017-09-11 19:00:09

  Mkutano wa 22 wa mwaka wa shirika la waendesha mashitaka wa kimataifa umefunguliwa hapa Beijing. Rais Xi Jinping wa China ametoa pongezi kufuatiakufunguliwa kwa mkutano huo.

  Katika pongezi zake Rais Xi amesema waendesha mashitaka wakiwa ni wawakilishi wa maslahi ya umma, wanabeba majukumu muhimu. Mkutano huo wenye kauli mbiu ya "uendeshaji wa mashitaka unahudumia maslahi ya umma", utajadili masuala mbalimbali yakiwemo kujenga jamii yenye usalama, haki na masikilizano inayotawaliwa kwa mujibu wa sheria, na kazi ya waendesha mashitaka katika kulinda maslahi ya umma, hivyo ni muhimu sana katika kusukuma mbele utawala kwa mujibu wa sheria katika nchi mbalimbali. China imepata uzoefu mkubwa katika mambo ya uendeshaji wa mashitaka na utawala kwa mujibu wa sheria, pia inapenda kujifunza uzoefu wa nchi nyingine. Amesema anatarajia waendesha mashitaka wa nchi mbalimbali watabadilishana uzoefu na kuimarisha ushirikiano kwenye mkutano huo ili kutoa mchango mpya kwa amani na maendeleo ya binadamu.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako