• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Mkutano wa 13 wa Umoja wa Mataifa kwa nchi zilizosaini mkataba wa kudhibiti kuenea kwa jangwa wafunguliwa

  (GMT+08:00) 2017-09-11 18:59:36

  Mkutano wa 13 wa Umoja wa Mataifa kwa nchi zilizosaini mkataba wa kudhibiti kuenea kwa jangwa umefunguliwa leo mjini Ordos, mkoani Mongolia ya Ndani, China.

  Rais Xi Jinping wa China amepongeza mkutano huo, na kusema kuenea kwa jangwa ni suala kubwa linaloathiri maisha na maendeleo ya binadamu. Kazi ya kudhibiti kuenea kwa jangwa imepata maendeleo tangu mkataba huo usainiwe katika miaka 21 iliyopita, lakini amesema katika baadhi ya sehemu duniani watu bado wanasumbuliwa na tatizo la kuenea kwa jangwa. Hivyo rais Xi amesisitiza kuwa kazi hiyo inahitaji ushirikiano wa jumuiya ya kimataifa, na China itashikilia kutekeleza majukumu yaliyoamuliwa na mkataba huo, kuimarisha mawasiliano na ushirikiano na nchi zilizosaini mkataba huo na mashirika ya kimataifa, ili kufanya juhudi pamoja na kujenga dunia nzuri zaidi.

  Katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa Bw. Antonio Guterres ametoa hotuba kwenye mkutano huo kwa njia ya video.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako