• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Wapiganaji 29 wa Taliban wauawa kwenye operesheni kubwa nchini Afghanistan

    (GMT+08:00) 2017-09-11 18:55:20

    Wizara ya Ulinzi ya Afghanistan imetoa taarifa ikisema takriban wapiganaji 29 wakiwemo makamanda wao watatu wameuawa na wengine 15 kujeruhiwa katika operesheni mfululizo zilizofanywa na vikosi vya usalama vya Afghanistan katika saa 24 zilizopita.

    Taarifa hiyo imefafanua kuwa vikosi vya ulinzi na usalama vilianzisha operesheni 13 za kusafisha na nyingine 17 katika majimbo 10 na kufanikiwa kukamata silaha na risasi ambazo baadaye ziliharibiwa na vikosi hivyo. Hata hivyo wapiganaji wa Taliban waliokuwa wakipigana na vikosi hivyo bado hawajatoa taarifa yoyote.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako